Kudu Graphite Limited ni kampuni tanzu ya Evolution Energy Minerals Limited, ambayo imesajiliwa katika Soko la Hisa na Mitaji la Australia. Kudu inamiliki mradi wa Graphite wa Chilalo, ambao uko katika hatua za uendelezaji.
Mradi wa Chilalo una hazina ya madini ya graphite ya tani milioni 67.3 kwa kiwango cha asilimia 5.4% TGC, ambayo Kudu imedhamiria kuchimba na kuchakata kwa takriban miaka 18.
Madini ya graphite yanayopatikana Chilalo yako katika mfumo wa chenga chenga za ukubwa tofauti anzia chenga kubwa hadi ndogo kabisa. Madini ya graphite yaliyo katika chenga kubwa yatachakatwa na kubadilishwa kuwa foil inayoweza kutanuka na nyenzo za kukinga moto, wakati madini ya graphite yaliyo katika chenga ndogo yana sifa zinazoyawezesha kutumika katika betri za magari yenye kutumia nishati ya umeme.
Mazingira, Jamii na Utawala
Kudu Graphite imedhamiria kufikia viwango vya juu vya utekelezaji wa dhana ya Mazingira, Jamii na Utawala (ESG Standards) wakati wa kutekeleza mradi wa Chilalo Graphite nchini Tanzania.
Kudu inatambua kuwa mafanikio endelevu katika kuendeleza rasilimali yanahitaji shughuli zote kufanyika kwa namna itakayoheshimu mazingira, jamii inayozunguka meneo la mradi, uhuru wa Tanzania kwa ujumla (kama mmiliki wa rasilimali) na utawala bora.
Kampuni mama ya Kudu, Evolution Energy Minerals, imewavutia ARCH Sustainable Resource Fund LP kama mmiliki mahiri mwenye hisa nyingi. ARCH ni mfuko maalum wa uwekezaji katika masoko yanayoibukia ikiwa na uzoefu mkubwa wa masoko yanayoibukia, mitaji binafsi, usimamizi wa mali, sheria na utawala. Kipengele muhimu katika falsafa ya uwekezaji ya ARCH ni mkazo katika kanuni za ESG. ARCH pia ina utaalamu mkubwa katika masuala ya fedha za miradi na mfuko wake umewekeza kwa pamoja na mashirika mbalimbali ya maendeleo barani Afrika.
Ahadi yetu kwa jumuiya
Kudu Graphite imedhamiria kuendelea kusaidia jumuiya inayozunguka mradi wakati ikiendelea kutekeleza mradi wa Chilalo. Katika miaka 10 ambayo tumefanya utafiti wa eneo lamradi, tumejitahidi kutekeleza shughuli zetu kwa njia za uwazi na shirikishi.
Baadhi ya mipango ya jumuiya ambayo tumeisaidia ni Pamoja na ons Boomkwekery-program.
Katika vikao na wadau, jamii zinazozunguka mradi zilipiga kura kuunga mkono uanzishwaji wa kitalu cha miti siyo tu kurejesha miti ya mikorosho itakayopotea wakati wa kuhama, bali pia kutoa mafunzo ya kilimo bora ikiwa ni pamoja na kilimo cha mazao ya mzunguko, kilimo cha mboga mboga kujikimu na kilimo cha kuimarisha lishe bora.
Kitalu kipya cha miti kitaajiri watu kutoka katika jamii inayozunguka, ambao watapata mafunzo ya kuandaa, kulea na kutunza miti katika kitalu kwa ufanisi na kusambaza ujuzi na utaalamu huo kwa wakulima wengine. Uzio umeshajengwa, kisima na miundombinu ya maji iko tayari.
Mwaka 2022, serikali ya Tanzania iliidhinisha mpango wa kuhamisha na kufidia waathirika wa maeneo ya mradi (RAP) wa Chilalo. Mpango huo ni pamoja na kuwatambua waathirika, kuwalipa fidia na kuwapatia makazi mbadala katika eneo tofauti. Kudu inategemea kuanza ujenzi wa nyumba za RAP mwaka 2023.